Jinsi ya Kutumia AI Kuboresha CV na CVBora
Kama mtafutaji kazi ambaye nna uzoefu wa zaidi ya miaka 10 na ujuzi unaofunika taaluma kama uhandisi majengo na miundombinu (Civil Engineering), uandishi wa programu za mitandaoni (Web Development), huduma kwa wateja (Customer Service), matangazo ya mitandaoni (Digital Marketing), na fani nyinginezo, nimepitia mengi ambayo yamenifanya nitengeneze CVBora.
Nimejifunza, kabla ya kupata nafasi ya kuonyesha ujuzi wako, inabidi kwanza CV na Cover Letter yako zivutie macho ya AI au binadamu anayepitia nyaraka hizi. Pamoja na hayo yote, kama huna "network", inabidi uapply kazi hata mia ndio uitwe kwenye interview.
Ili kurahisisha kazi kwako na kukuongezea nafasi ya kupata angalau interview, tumia CVBora.
CVBora ni tovuti inayotumia AI ya kisasa ya Gemini 3.1 Pro Preview kupitia CV yako ya zamani, ukurasa wako wa LinkedIn, au kukufanyia interview, kisha hutengeneza CV mpya ya kisasa kuendana na kazi unayoomba. Angalia mfano wa picha hapo chini.



Pamoja na kukutengenezea CV na Cover Letter ndani ya dk 1. CVBora inaweka kumbukumbu ya CV na Cover Letter zote ilizowahi kukutengenezea.

CVBora inakupa CV na Cover Letter 2 bure kwa siku, na baada ya hapo ni sh 200 tu kutengeneza zaidi!
Unaweza kujaribu CVBora hapa!
Comments (1)
Log in to post a comment.
Wow, really?!!